.

.

06 Agosti 2015

RAIS KIKWETE AMEWAAGA WATUMISHI WA MAHAKAMA AKIWATAKA KUKAMILISHA MASHAURI YA UCHAGUZI

Rais Jakaya Kikwete amewaaga rasmi watumishi wa mahakama kwa kuwataka wayakilize na kuyakamilisha kwa haraka mashauri yanayohusu uchaguzi yatakayofikishwa mahakamani, ili kuweza kutoa haki kwa walengwa kwa wakati.
Akizungumza na watumishi hao jijini Dar es salaam Rais Kikwete amesema siyo vema shauri lililofikishwa mahakamani likate muda mrefu bia kuamuliwa mpaka mtu anayelalamikiwa anamaliza kipindi chake cha uongozi na shauri bado halijaisha.
 
Aidha, ameitaka mahakamana kutenda haki kwa wananchi, kwani isipofanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wakatumia nguvu kuipata haki yao, jambo ambalo linaweza kusababisha amani kuvunjika.
 
Kwa upande wake, Jaji Mkuu Mheshimiwa Othumani Chande amempongeza Rais Kikwete kwa namna alivyotoa kipaumbele katika eneo la mahakama na kusema kuwa yapo mambo mengi mazuri yamefanyika kwa kipindi hiki cha miaka kumi cha utawala wake ikiwemo kuongeza idadi ya wafanyakazi wa idara hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni