Chifu
Lutalosa Yemba ameteuliwa kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha Alliance for Democratic Change (ADC)
Mkutano
mkuu wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) umemteua Chifu
Lutalosa Yemba kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
mwenyekiti wa chama hicho, Said Miraaj Abdulla kuwa mgombea mwenza.
Mkutano
huo pia ulimpitisha Hamad Rashid Mohamed kuwania urais wa Zanzibar na
kuahidi iwapo hatatekeleza ahadi zake kwa wananchi, akimaliza miaka
mitano afungwe jela miezi sita kama adhabu ya kudanganya.
Kuteuliwa
kwa Chifu Yemba kuwania urais wa Tanzania kunafanya wagombea wa nafasi
hiyo ya juu katika siasa nchini kufikia saba baada ya Chadema kumteua
Edward Lowassa mapema wiki hii na Chauma kumteua Hashim Rungwe.
Wagombea
wa vyama vingine ambao walishapitishwa na tayari wamechukua fomu kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni Dk John Pombe Magufuli wa CCM, Fahmi
Dovutwa (UDPD), Mchungaji Christopher Mtikila (DP) na Maxmillian Lyimo
(TLP
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni