Ni sauti pekee iliyokuwa ikisikika kwa saa takribani saa 4, huku
wengi wakiwa na shauku ya kujua nini mwenyekiti wa chama hicho alitaka
kuzungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Buguruni
Dar es Salaam.
Baada ya kusubiri kwa muda wa kutosha makao makuu hapo, hatimaye Bi
Magdarena Sakaya ambaye ni naibu katibu mkuu wa CUF bara akatangaza
kuahirisha mkutano huo.
Aidha ITV ilifanikiwa kuzungumza na badhi ya wanachama hao
waliokuwa wamejawa na jaziba amapo pamoja na masuala mengine alikuwa na
haya ya kuzungumza
Hata hivyo wakati alipokuwa akihutubia mkutano mkuu wa chadema
katibu mkuu wa CUF Malim Seif Hamadi alisema kuwa hana taarifa zozote za
kutaka kujiuzulu mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahimu Lipumba.
Kwa siku kadhaa kumekuwa na habari ambazo hata hivyo
hazijathibitishwa zikidai kuwa huenda mwenyekiti huyo akajiuzulu muda
wowote kaunzia sasa kutokana na madai ya kutokuelewana na baadhi ya
wakurugenzi wa chama huku taarifa nyingine ambazo pia si rasmi zikisema
kuwa ni kutokana na maamuzi ambayo si shirikishi ya kumapta mgombea wa
urais wa Ukawa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni