Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama cha Alliance for
Democratic Change, mgombea urais wa tiketi ya ADC Zanzibar Bwana Hamad
Rashid amehasa watanzania kutambua kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu
unagubikwa na gilba nyingi zikiwemo za matumizi makubwa ya fedha hali
inayohatarisha mfumo wa domkrasia katika uchaguzi wa viongozi.
Kwa upande wake mgombea wa Tanzania urais tiketi ya chama cha ADC
Bwana Chifu Luta Hiyemba amesema ameilalamikia serikali kwa kuingilia
mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na baadhio ya taasisi kushindwa
kudhibiti matumizi ya fedha katika kampeni za siasa za vyama mbalimbali
hali inayoendelea kusababisha kupatikana viongozi wanaopenda mamlaka
zaidi kuliko kutatua matatizo yanayowakabili watanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni