Siku
chache zilizopita Rekodi ya mtu mfupi zaidi Duniani ilibaki wazi,
aliyekuwa anashikilia Rekodi hiyo, Chandra Bahadur Dangi raia
wa Nepal alifariki akiwa na umri wa miaka 75.. lakini Guinness World
Records wameipata
rekodi
nyingine ya kuvutia.Hawa ndio wapenzi warefu zaidi Duniani, majina yao
ni Sun Mingming, mwanaume mwenye umri wa miaka 33 na mpenzi wake, Xu
Yan ambaye ana miaka 29 wote ni Raia wa China.. uhusiano wao ulianza
walipokutana kwenye Mashindano ya Michezo ya Kitaifa China mwaka 2009,
mwanaume ni mchezaji wa Basketball na mwanamke ni mchezaji wa handball.
Baada ya
mambo kwenda sawa pande zote, walifunga ndoa mwaka 2013 na wako pamoja
mpaka sasahivi, maisha yanaendelea poa japo moja ya changamoto kubwa
wanayokutana nayo ni pale wanaposafiri kwenye basi, au ndege kupata siti
za kuwatosha ni tatizo !!
Sun na
mpenzi wake siku ya Ndoa yao.Sun na mpenzi wake Xu wako Makao Makuu
ya Guinness World Records ndani ya Uingereza ambapo rekodi yao
itaingizwa pia kwenye Kitabu cha Rekodi za Guinnesskitakachotoka mwaka
2016.
Sun
Mingming ana urefu wa futi 7.8 alafu mkewe ana urefu wa futi 6.1,
kilichofanywa ni kuujumlisha urefu wao kwa pamoja ambapo jumla yake
inakuwa Futi 13.10 !!Kipande cha video yao hiki hapa pia mtu wangu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni