Ijumaa, Januari 22, 2016
Gazeti la
Jamhuri lapewa siku saba kukanusha habari iliyoandikwa kwenye gazeti
hilo Januari 18, 2016 toleo no. 25 lililokuwa na kichwa cha habari
FAMILIA YA JK YAHUSIKA UDA habari iliyokuwa ukurasa wa mbele wa gazeti
hilo.
Hayo yamesemwa
na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simos Group na UDA, Robart Kisena
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo,amesekuwa hakuna uhusiano wa umiliki na familia ya Rais Mstaafu wa
Awamu ya Nne,Dk Jakaya Kikwete.
Kisena amesema
kuwa Familia ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
hahusiki kabisa kwani kampuni ya UDA na kampuni ya Simon Kisena
haihusiani na familia ya JK hata miradi inayofanywa na Kampuni hiyo.
Aidha amesema
gazeti lililoandika habari hiyo linatakiwa kuomba radhi kwa siku hizo
kwa kuwa na habari yenye uzito ule ule na ukurasa ule ule.
Kisena amesema
wasipofanya hivyo watapelekwa mahakamani ili wakatoe ushaidi wa
maandishi mahakamani hapo juu ya uhusikaji wa Familia ya Rais Mstaafu
katika kampuni ya usafiri Dar es Salaam (UDA).
Hata hivyo
amesema kuwa kampuni ya (UDA) itarudishwa kwa wananchi ifikapo Machi
Mwaka huu ili iweze kuendeshwa kwani shirika hili kwa mara ya kwanza
lilikua na magari 7 mpaka sasa maari hayo yameongezeka na kufikia zaidi
ya magari 400.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni