Ijumaa, Januari 22, 2016
Kamanda mkuu wa
kundi la wanamgambo la Alshabab, Maalim Janow, auawa baada ya kupata
shambulio la anga kutoka kwa wanajeshi wa Kenya, Mkuu wa majeshi nchini
Kenya Jenerali Samson Mwathethe aliuambia mkutano wa wanahabari mjini
Nairobi.
akirejelea
mauaji ya wanajeshi wa Kenya nchini Somali na wanamgambo wa Alshabab,
Jenerali huyo alisema kuwa bomu lililotumika na wapiganaji hao ni mara
tatu kwa ukubwa wa lile lililotumika katika ubalozi wa Marekani jijini
nairobi mwaka 1998 ambalo liliangusha jumba la ghorofa 10 na kuua zaidi
ya watu 200 na kujeruhi wengine 5000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni