Kikosi
cha Ruvu Shooting ya Pwani, jana Jumapili ilifanikiwa kuwa timu ya
kwanza kupanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya kuibuka
na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli na kufikisha pointi 31 ambazo
haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye Kundi B.
Ruvu
ambayo ilishuka daraja msimu uliopita, jana iliingia uwanjani ikiwa
tayari imeshajikatia tiketi ya kucheza ligi kuu msimu ujao kutokana na
timu iliyokuwa ikiifukuzia kwa ukaribu ya Njombe Mji kufungwa katika
mchezo wa mapema kwa bao 1-0 na JKT Mlale na kubaki na pointi 20 ambazo
kwenye mechi mbili zilizobaki hawezi kumfikia Ruvu.
Tayari
Ruvu imepanda, lakini hali imekuwa tofauti kwa makundi mengine ya A na C
ambayo mpaka sasa hakuna timu iliyojihakikishia kupanda daraja.
Haya
ndiyo matokeo mengine ya mechi za jana za ligi hiyo: Polisi Dodoma 1-2
Africa Lyon, Friends Rangers 3-1 Ashanti United, Polisi Dar 0-2 KMC FC
na Polisi Tabora1-0 Geita Gold.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni