Daktari wa
hospitali ya Mayo ya jimbo la Minnesota, Marekani ametoa ripoti ya
utafiti akisema, kitambi kina hatari kubwa zaidi kuliko unene.
Ripoti hiyo
imesema, kutokana na takwimu za wagonjwa elfu 15, hatari ya kufariki ya
wanaume wenye vitambi ni maradufu ya wanaume wanene wa kawaida, na
hatari ya kufariki kwa wanawake wenye vitambi ni mara 1.5 ya ile ya
wanawake wanene wa kawaida.
Chanzo cha
ongezeko la hatari hiyo ni kuwa kitambi kinaweza kuongeza mafuta ndani
ya mwili, na maini yatayabadilisha mafuta hayo kuwa lehemu
(cholesterol). Lehemu hiyo inaingia katika mishipa ya damu na
kusababisha kiharusi na magonjwa ya moyo.
Utafiti wa awali
pia ulionesha kitambi kinaongeza hatari ya ugonjwa wa kisukari,
kiharusi, magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo na ubongo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni