Kundi la wanamgambo IS linadaiwa kuhusika na shambulio hilo
Takriban
watu 50 wameuawa kwa mlipuko wa bomu karibu na hekalu la kishia la
Sayyida Zeinab,kusini mwa mji wa Damascus nchini Syria.
Kituo cha
basi na Jengo lililo na makao makuu ya jeshi vilishambuliwa na milipuko
ambayo iliharibu magari yaliyokuwepo katika eneo hilo.
Ilitokea
wakati Serikali na makundi ya upinzani walipokutana mjini Geneva kwa
ajili ya mazungumzo yenye kulenga kupata suluhu ya kisiasa kuhusu mzozo
wa nchini humo.
Shambulio
hilo linadaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State, ambalo linaelezwa
kulenga kuvuruga mazungumzo hayo, Umoja wa Ulaya umeeleza.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amezisihi pande zote mbili kukomesha vitendo vya umwagaji damu.
Mjumbe wa Umoja wa mataifa nchini Syria amepanga kufanya mazunguzo na pande mbili mjini Geneva, Jumatatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni