Mamlaka nchini
Uingereza zimebaini kwamba zaidi ya wasichana 1,000 ambao ni raia wa
Uingereza wenye asili ya Afrika magharibi wanachomwa na jiwe lenye moto
kwa matiti yao kama njia ya kuwazuia kupunguza hisia za kingono.
Gazeti la Daily
mail linasema wanaofanya vitendo hivyo wanatumia vifaa kama nyundo na
mawe moto wakiamini itapunguza hamu ya mapenzi kwa wasichana na hivyo
kuepusha mimba za mapema.
Wanaamini pia matiti yao hayatakuwa makubwa na hivyo hayatavutia wanaume.
Tamaduni hiyo ilitokea Cameroon ambako kila msichana mmoja kati ya wanne anaathirika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni