Aliyekuwa
Mwenyekiti wa chama cha Demokrsaia na Maendeleo Chedema mkoa wa Mwanza
Andrian Tizeba, leo amejiunga rasmi na CCM wilayani Sengerema tawi la
Lugata.
Tizeba
ambaye alitangaza kujivua uanachama wa chadema Machi 29 mwaka huu baada
ya kusimamishwa uongozi kwa muda wa mwaka mmoja, na kutangaza kuachana
na siasa, amekabidhiwa kadi hiyo na katibu wa tawi hilo Alfred
Mwambala.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Tizeba amesema uamuzi wake si wa kulazimishwa na mtu
bali, ameona ni vema arudi kwenye chama chake cha awali.
Tizeba
ambaye ni kaka wa mbunge wa jimbo la Buchosa, Charles Tizeba amesema,
nia na dhumuni la kujiunga na chama hicho ni kutokana na utendaji wa
Rais John Magufuli anaoufanya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni