Zaidi ya shule
130 jijini Bengaluru, nchini India zimefungwa baada ya chui watatu
kupatikana wakirandaranda ndanii ya mojawapo ya shule hizo katika
kipindi cha siku tatu zilizopita.
Siku ya Jumapili
chui mmoja alipatikana akirandaranda ndani ya shule ya Vibgyor na siku
mbili baadaye wengine wawili wakapatikana karibu na shule hiyo hiyo.
Mmoja wa chui hao alishikwa na maafisa wa wanyamapori lakini wengine
wawili bado hawajulikani waliko.
"Kufuatia tishio
la chui tumefunga shule 134 katika jiji la Bengaluru. Tutatoa uamuzi
iwapo tutazingua Ijumaa," afisa wa serikali ambaye hakutaka kutambuliwa
alisema. Visa vya chui kupatikana ndani ya maeneo panapoishi watu
vimeongezeka nchini India ambapo kuna zaidi ya chui 14,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni