Kesho
Jumapili May 1, utapigwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) kati
ya Simba SC vs Azam FC kwenye uwanja wa taifa.
Mechi
hiyo ni muhimu kwa vilabu vyote kwasababu itaamua ni klabu ipi itaendelea na
mbio za ubingwa huku ile itakayofungwa ikipoteza matumaini ya kutwaa taji hilo
ndani ya msimu huu. Mechi hii unaweza kuiita ya kufa na kupona ama fainali ya
kuamua nani ataendelea kuifukuza Yanga katika kuwania ubingwa wa msimu huu
2015-16.
Kuelekea
mchezo huo, nakuhabarisha mechi nne (4) zilizopita ambazo zitaendelea
kukumbukwa na wadau na wapenda soka Tanzania.
- Simba 0-2 Azam FC: Okt 4, 2008
Hii ni
mechi ya kwanza kabisa baina ya timu hizi. Mechi hii ni ya kukumbukwa kwa
sababu baada ya mpira kuisha, wanachama wa Simba waliandamana mpaka nyumbani
kwa mwenyekiti wao Hassan Dalali wakimtaka awaachie timu yao. Dalali akatii
amri, akatangaza kujiuzulu. Siku chache baadaye wanachama wengine wakaenda
kumuomba afute uamuzi wake naye akakubali kwa kusema alikuwa anapima maji kama
anapendwa au la. Kitendo cha kufuatwa na kuombwa arudi kwenye nafasi yake ya
uongozi kilimridhisha kwamba anapendwa hivyo akarudi uongozini.
- Azam 0-3 Simba: Machi 30, 2009
Mechi
hii itakumbukwa kwa kuchezwa siku mbili. Siku ya kwanza mchezo ulivunjika
wakati wa mapumziko kutokana na mvua kubwa kunyesha. Mpaka mchezo
unavunjunjika, Simba walikuwa wakiongoza 1-0 goli lililofungwa na Ramadhani
Chombo ‘Redondo’ dakika ya 33.
Mashabiki
wa Yanga walikuwa wakiwadhihaki wenzao wa Simba kwamba wamezoea uchawi wa mvua
wakirejea kuvunjika kwa mchezo wa Simb
a na Ismailia 2001 kombe la CAF.
Mechi
iliporudiwa, Simba walishinda 3-0 huku beki wa Azam FC Cyprian Odura akipewa
kadi nyekundu. Baada ya mchezo, kocha wa Azam FC Neider Dos Santos alimshukia
nyota wake aliyempiga benchi siku hiyo, Shaaban Kisiga Malone, akisema nyota
huyo hatakiwi kujiona ‘staa’ sana kwa sababu Tanzania hakuna staa kwani hakuna
hata mchezaji mmoja aliyecheza fainali za kombe la dunia. Akaongeza
kwamba anataka kuiandaa Azam FC ya baadaye itakayoanza kutoa matunda mwaka 2010
kupitia chipukizi wake kama Himid Mao na Tumba Sued.
- Simba 3 -1 Azam FC: Okt 27, 2012
Mchezo
huu utakumbukwa kwa kuchafua hali ya hewa klabuni Azam FC. Kwamza uligharimu
kibarua cha kocha Boris Bunjak na baadaye kitambaa cha unahodha cha Aggrey
Morris.
Aggrey
na wachezaji wenzake, Deogratias Munishi ‘Dida’, Said Morad na Erasto
Nyoni walisimamishwa wakihusishwa na kupokea rushwa ili kuihujumu klabu hiyo kwenye
mchezo huo.
Huu
ulikuwa msimu ambao Azam FC walipania kiukweli kutwaa ubingwa wa ligi kuu hasa
baada ya kujipima kwenye mashindano ya Kagame 2012 na kufika fainali. Mtu
aliyetarajiwa kufanikisha mpango huo alikuwa kocha Boris Bunjak kutoka Serbia.
Azam
iliuanza vyema msimu huu lakini kizunguzungu kilianza baada ya kipigo cha 2-0
kutoka kwa Yanga. Licha ya kwamba walirudi kwa kishindo na kushinda michezo
miwili mfululizo, 1-0 vs African Lyon na tena 1-0 dhidi ya Polisi Moro, Azam FC
walijikuta wakiyumba na kutoa sare mbili mfululizo 0-0 vs TZ Prisons na 1-1 vs
Ruvu Shooting. Mpaka hapo matumaini ya ubingwa yakaanza kupotea na ndipo kikaja
kipigo hiki kilichoumiza mashabiki wake wengi. Shabiki mmoja aliyeitwa Hamisi
Shaku aliandika kwenye ukurasa wa Facebook wa Azam FC, “FT: Simba 3-1 Azam FC,
Hata siamini kama tumefungwa goli zote izo…..daah come one Azam Tunaumia
mashabiki wenu….kazeni bwana msikate tamaa”.
- Azam 2 -1 Simba. Machi 30, 2014
Mchezo
huu utakumbukwa kwa kitendo cha mashabiki wa Yanga kuishangilia Simba huku
mashabiki wa Simba wakiiacha timu yao na kuishangilia Azam FC.
Huu
ulikuwa msimu ambao mbio za ubingwa ziliitenga Simba na kuwaacha Azam FC
wakichuana na Yanga.
Azam FC
walikuwa mbele ya Yanga kwa pointi nne na Yanga waliitegemea mechi hii kwamba
Azam FC wateleze ili pengo lipungue.
Azam
walianza kupata bao kupitia Mcha Khamis na kushangiliwa sana na mashabiki wa
Simba. Beki wa Simba Joseph Owino aliisawazishia timu yake na kuamsha shamra
shamra kwa mashabiki wa Yanga huku wale wa Simba wakinuna. John Bocco
akaifungia Azam FC bao la pili akiunganisha kwa kichwa ‘rebound’ ya tik-tak ya
Kipre Tchetche na kuwainua vitini mashabiki wa Simba. Sherehe kwa mashabiki wa
Simba zilikuwa kubwa zaidi pale taarifa zilifika uwanjani humo kutoka Tanga kwamba
Yanga walifungwa 2-1 na Mgambo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni