.

.

04 Aprili 2016

WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO ASISITIZA SWALA LA VIINGILIO VYA MPIRA WA MIGUU KATIKA VIWANJA VYA MPIRA WA MIGUU.

 




Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh Nape Moses Nnauye amesisitiza swala la siasa si lakulileta katika michezo.
akizungumza na wana habari katika uwanja wa sokoine mkoa wa Mbeya
Nauye amesema kwa kufanya hivyo kutasababisha kuiharibu Timu ya Mbeya city fc amabayo ilifanya vizuri msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara,na kuoneshea mfano wa timu ya Mbeya city na kusema waliingiza siasa ndio maana timu ipo nafasi mbaya hivyo na kuiua kabisa waiache iwe timu ya wananchi, Inayo milikiwa na halamshauri ya jiji.

“Nimesikia kuna wanasiasa wanaingiza siasa katika Timu hii naomba waache mala moja kwani mkiruhusu siasa kwenye mpira mtaipoteza timu yenu.

Kuweni makini sana na wanansaiasa wananchi wa mbeya Timu yenu itakufa kwakua mala nyingi sisi wanansiasa tunaleta itikadi tofauti katia timu” amesema Nauye

Ameongeza kua watuimie Timu hiyo kuwaunganisha na kuwaleta pamoja wananchi  lakini si kuingiza mambo ya siasa yatakayo wagawa.
 
Hayo yalisemwa  siku ya tarehe mbili wakati mpambano  wa mpira wa miguu ligi kuu Tanzania bara kati ya timu ya Mbeya city fc na Coastal Union ya Tanga mchezo uliochezwa katika dimba la uwanja wa kumbukumbu wa sokoine ambapo Mbeya city fc iliibuka ushindi wa magoli manne kwa sifuri.

Nape Moses Nnauye pia aliweza kusisitiza swala la viingilio katika viwanja vya mpira wa miguu huku akizungumzia swala la mashine za electroniki.kuaanza kutumika katika katika baadhi ya viwanja,huku akisisitiza swala la kusimamia ipasyo swala la viingilio na usimamizi wa pesa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni