Nimechagua safu
nzuri na tutaendelea kuchaguana, wakafanye kazi. Najua wengine bado
sijachagua, na wengine wanakuwa na wasiwasi. Kama wewe ni mfanyakazi,
uko DC au Mkurugenzi, una wasiwasi gani? Tena unapozidi kuwa na
wasiwasi, ndiyo uwezekano wa kutolewa unakuwa mkubwa. Ni lazima
niwaambie waheshimiwa maDC, ukiwa na wasiwasi hutafanya kazi. Na sisi
tutakuona wewe hufanyi kazi. Utaondoka tu. Ukiwa Mkurugenzi ukawa na
wasiwasi, huo wasiwasi ndiyo dalili nzuri ya kukufanya wewe uondoke.
Fanya kazi. Chapa kazi kwa ajili ya Watanzania hawa. Watakuona tu. Hata
mimi sitakuwa Rais maisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni