Na Mwene Said, Dar.
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa
Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani.
Meya
huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia mwandishi wa Habari wa
gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali.
Kesi
hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya
usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja.
Wakili
wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa
lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani.
Kutokana
na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa
huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri
hilo.
Hakimu
alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya
huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya
usikilizwaji.
Katika
kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 11, mwaka jana,
maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam, kipindi hicho akiwa na cheo cha
Udiwani kata ya Ubungo.Ilidaiwa kwamba,mshitakiwa huyo alimpiga Lissa
kwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia
majeraha makali.
Shitaka
la pili ilidaiwa kwamba ,mshitakiwa huyo katika tarehe hiyo kwa
makusudi na kinyume cha sheria aliharibu kamera aina ya Nicon yenye
thamani ya sh. milioni nane mali ya Kampuni ya Uhuru Publication
Limited.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni