Jumatatu, Januari 25, 2016
Watu zaidi ya 50 wamefariki nchini Taiwan kutokana na wimbi la baridi kali ambalo limeathiri maeneo ya Asia Mashariki.
Watalii zaidi ya 60,000 pia wamekwama Korea Kusini kutokana na kibaridi hicho.
Vyombo
vya habari nchini Taiwan vinasema vifo hivyo vimetokana na kushuka sana
kwa kiwango cha joto mwilini na wengine wakafariki kutokana na maradhi
ya moyo.
Hii ni baada ya viwango vya joto kushuka ghafla wikendi.
Hayo yakijiri,
theluji nyingi imesababisha kufungwa kwa uwanja wa ndege katika kisiwa
cha Jeju nchini Korea Kusini, ambacho ni maarufu sana kwa watalii.
Safari za ndege zimekatizwa.
Wimbi hilo la baridi limeathiri sana Hong Kong, Uchina kusini na Japan.
Walioathirika zaidi Taiwan ni wazee wanaoishi maeneo ya kaskazini kama vile Taipei, Kaohsiung na Taoyuan.
Katika baadhi ya maeneo ya Taiwan, viwango vya joto vilishuka hadi nyuzi 4C (39F) siku ya Jumapili.
Hong Kong, hali
ilikuwa mbaya zaidi, baadhi ya maeneo yakishuhudia vipimo vya joto vya
nyuzi 3C, kikiwa ndicho kiwango cha chini zaidi kushuhudiwa eneo hilo
katika kipindi cha miaka 60.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni