Mtoto wa
miaka mitatu aliyefahamika kwa jina la JANET PONSIAN mkazi wa Matemela Wilaya
ya Mbarali Mkoani Mbeya alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na Gari
yenye namba za usajili T.957 CWJ aina ya Isuzu Journey ikiendeshwa na dereva
aliyefahamika kwa jina la ELIABU MYEKO (33) mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe.
Tukio hilo
limetokea mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:45 jioni huko katika Kijiji
cha Matemela, Kata ya Ipwani, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa
Mbeya.
Aidha
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa Dereva wa Gari hilo. Dereva
alikimbia mara baada ya tukio na jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na
mmiliki wa Gari zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Kituo cha Afya
Ipwani Wilayani Mbarali kwa uchunguzi wa kitabibu.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA
anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni
pamoja na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka
ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa
zitakazofanikisha kukamatwa kwa dereva huyu azitoe kwa mamlaka husika ili
akamatwe.
Katika
Misako:
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Matemela aliyefahamika
kwa jina la HUSSEIN BAKARI (59) baada ya kukutwa na miche 25 ya Bhangi akiwa
amepanda kwenye bustani yake ya mbogamboga.
Mtuhumiwa
alikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.02.2016 majira ya saa 16:00
jioni katika Kijiji cha Mayota, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya
Mbarali, Mkoa wa Mbeya.
Aidha
katika msako mwingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la WILSON PHILIP (19)
mwendesha Pikipiki @ bodaboda, mkazi wa Msasani anashikiliwa na Jeshi la Polisi
Mkoa wa Mbeya akiwa na Bhangi yenye uzito wa Gram 10.
Mtuhumiwa
alikamatwa na askari katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya
saa 17:05 jioni huko Mtaa wa msasani, Kata ya Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Mjini,
Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Watuhumiwa
watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamiliki.
Imesainiwa
na:
(EMANUEL
G. LUKULA – ACP)
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni