Mama
mmoja amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua katika hospitali ya Rufaa
Meta ya jijini Mbeya na baada ya kujifungua muuguzi huyo akamchukua mwanae
mchanga na kumtupia kifuani jambo ambalo amesema lilihatarisha uhai wa mwanae.
Mkuu wa
mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amefanya ziara ya kustukiza katika hospitali ya
Rufaa ya wazazi Meta ya jijini Mbeya na kushuhudia msongamano mkubwa wa akina
mama wajawazito hospitalini hapo, na alipofika katika chumba cha akina mama
ambao wanasubiri watoto wao ambao wamewekwa katika chumba maalum cha joto,
ndipo akakutanana na malalamiko ya mama Salome Waya ambaye amedai kupigwa na
muuguzi wakati akijifungua.
Kufuatia
madai hayo, mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akalazimika kupitia nyaraka za
mama huyo ili kumtambua muuguzi aliyemfanyia ukatiri huo na akafanikiwa
kumbaini kuwa anaitwa Beatrice Sanga ndipo akatoa agizo kwa mkurugenzi wa
hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini, Dk. Goodlove Mbwanji
kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo ndani ya siku saba.
Mkurugenzi
wa hospitali hiyo, Dk. Goodlove Mbwaji amesema kuwa katika mazingira hayo
hawezi kujitetea na badala yake atazingatia maelekezo ambayo amepewa na mkuu wa
mkoa.
CREDIT FAHARI NEWS
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni