.

.

18 Juni 2016

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA JUNE 18, 2016


Mshambuliaji Neymar Yupo Mbioni Kusaini Mkataba Mpya na Barcelona na Kuvitosa Vilabu Vikubwa Barani Ulaya Vinavyohitaji Saini Yake Wakiwemo Manchester United na PSG (Daily Mirror), Uongozi wa Klabu ya Leicester City unaamini Kuwa Mshambuliaji wao Jermie Vardy atasalia ndani ya klabu hiyo na Kukataa Ofa ya Pauni Milion 20 kutua Arsenal
, Wakati huo huo klabu ya Arsenal imeingia kwenye mbio za kusaka saini ya Mshambuliaji wa Spurs Mousa Dembele (Daily Star), Real Madrid wapo mawindoni Kusaka saini ya kiungo wa Leicester City N’golo Kante(Daily Star), Wakati Matajiri wa Ufaransa PSG Wanatarajia Kufanya Uhamisho wa Mshambuliaji Romelu Lukaku Kutoka Everton(Daily Mail) , Kocha Mpya wa Manchester United Jose Morinho anataka Kumsajili Kiungo wa Wolfburg Mjerumani Julian Draxler. (Daily Star), Kocha wa Chelsea Antonio Conte anataka Kumsajiri Mshambuliaji wa Liverpool Christian Benteke ili Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji (The Times) , Tottenham Wapo Kwenye Makubaliano na Watakatifu Southampton ya Kumsajili Kiungo wa Southampton Victor Wanyama (Sky sources), Feyenoord wamekamilisha Usajili wa Nicolai Jorgensen kutoka FC Copenhagen kwa Mkataba wa Miaka Mitano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni