Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita
ambao ni majirani wa Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu ya GGM mkoani humo.
Wananchi hao wamelalamika kuwepo na vitendo vya ukatili dhidi yao
vinavyofanywa na baadhi wa askari wa kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi
Masauni aliwataka Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi
ya tuhuma hizo.
Mkazi
wa Kijiji cha Nyakabale, Kata ya Mgusu, mkoani Geita, Biosi Makongoro
akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kushoto aliyekaa) dhidi ya Kampuni ya Uchimbaji wa
Dhahabu ya GGM mkoani humo ambayo ipo jirani na kijiji hicho, kuwa
askari wa kampuni hiyo wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi hao wanapopita
katika eneo la Kampuni hiyo. Hata hivyo Mhandisi Masauni aliwataka
Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka dhidi ya tuhuma hizo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akiwasili Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani
Bukombe ambacho Mbunge wa Jimbo hilo, Dotto Biteko aliuliza swali la
nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho kinahitaji
matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya ziara jimboni
kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema Serikali yake
itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.
Mkuu
wa Kituo cha Polisi Runzewe kilichopo Kata ya Uyovu wilayani Bukombe,
Jackson Kirahuka akimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa koti) sehemu mbalimbali za
kituo hicho ambacho Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dotto Biteko (katikati)
aliuliza swali la nyongeza Bungeni hivi karibuni akisema kituo hicho
kinahitaji matengenezo makubwa na kumuomba Naibu Waziri huyo kufanya
ziara jimboni kwake kujionea kituo hicho. Hata hivyo, Masauni alisema
Serikali yake itahakikisha kituo hicho kitakuwa katika hali nzuri.
Aliyevaa Kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Amani Mwenegoha.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili
kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali,
Mstaafu Ezekiel Kyunga (meza kuu), Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,
Joseph Msukuma (kulia), na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli
Mwabulambo, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani
humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia
jambo Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma (watatu kulia),
na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Mponjoli Mwabulambo (wapili
kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi mkoani
humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akitoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukendo, Amani Mwenegoha (kushoto)
mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
hiyo iliyopo mkoani Geita. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi mkoani
Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni