Serikali imeagiza Maafisa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mikoani kuanza kushirikishwa katika vikao vya maamuzi ili wapate kujua mikakati ya maendeleo kwa sekta zao.
Agizo hilo limetolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Annastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi Jijini Tanga kwa ambapo lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kisekta kwa Wizara yake katika Mkoa huo.