.

.

03 Aprili 2015

NEMC yatoa saa 24 kwa wamiliki wa viwanda Morogoro....

Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira NEMC imetoa saa 24 kwa wamiliki wa kiwanda vya nguo vya 21st Century na kiwanda cha ngozi cha AC Limited kuhakikisha wanazuia maji machafu yanayotiririshwa katika makazi ya wananchi vinginevyo watavifungia uzalishji wa viwanda hivyo. Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira NEMC Dr Robert Ntakamulenga ametoa agizo hilo kufuatia ukaguzi uliofanywa na wataalam ukiongozwa na mkuu wa wilaya ya Mvomero Bw Festo Kiswaga ambapo wamejionea maji machafu yaliochanganyika na kemikali za sumu yakitiririswha katika makazi ya wananchi ambapo ametoa saa 24 kwa wamiliki wa viwanda hivyo kukubailiana jinsi ya kudhibiti mfumo wa utiririshaji wa maji machafu.
Hata hivyo kumekuwa na mvutano kuhusu kiwanda kipi kinahusika kumwaga maji machafu ambapo wamiliki hao wa viwanda wakizungumzia maagizo ya NEMC meneja wa kiwanda cha ngozi cha AC David Dismas amesema wanayafanyia kazi maagizo hayo huku meneja wa kiwanda cha 21Century Clement Munisi amesema tayari wameanzaisha mfumo mpya wa kutoa maji machafu kwa kutumia mirereji mpya walioujenga na tayari umeanza kufanya kazi.
Nae mwenyekiti wa mtaa wa kilima hewa Msajigwa Mwakiruma amesema wananchi wameridhika na hatua zilizochukuliwa na NEMC kwani kasi ya maji kuingia katika makazi ya wananchi imepungua huku mkaguzi wa mazingira katika manispaa ya Morogoro Tomasi Ngaila amesema wataendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha viwanda hivyo vinafuata makubalinao waliofanya na NEMC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni