.

.

01 Mei 2015

TANROADS IMEWAFUKUZA WATUMISHI WAKE KUTOKA KITENGO CHA MIZANI.

Wakala wa Barabara nchini Tanzania – TanRoad, imewafukuza kazi zaidi ya watumishi wake mia nne kutoka kitengo cha mizani zilizopo kwenye barabara kuu nchini kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli, amesema hayo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wake na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, mkutano ambao pia amewataka watendaji walio chini yake kutoogopa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wazembe na wala rushwa.
Kwa mujibu wa waziri Magufuli, hatua hiyo itaongeza ufanisi katika utendaji wao ambapo ametolea mfano jinsi hatua ya Tanroad ilivyopandisha rekodi ya utendaji wa taasisi hiyo kiasi cha kuibuka kuwa ya tatu barani Afrika baina ya wakala zenye jukumu la usimamizi wa miundombinu ya barabara

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni