.

.

26 Juni 2015

MUSWADA WA HABARI WAONDOLEWA BUNGENI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (asiye na wizara maalum) Prof Mark Mwandosya ameliambia bunge leo asubuhi kuwa serikali imefikia uamuzi huo kutokana na maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya maendeleo ya jamiii iliyotaka musawada huo uondolewe ili kutoa muda wa kujadiliwa na wadau.
Katika taarifa yake hiyo kwa Bunge Mh. Mwandosya amewataka wadau wa habari waendelee kutoa ushauri juu ya muswada huo pamoja na kuchangia maoni zaidi ili kupata muswada ulio bora zaidi.
Prof Mwandosya amesema muswada huo utawasilishwa na kujadiliwa katika mkutano ujao wa bunge ambao utakuwa ni wa bunge la kumi na moja chini ya serikali ya awamu ya tano.
Uamuzi huo wa serikali umekuja kutokana na muswada huo kuzusha mgogoro na wadau wa tasnia ya habari baada ya kuonekana kutowashirikisha wadau wa habari moja kwa moja lakini pia kuonekana inaminya uhuru wa wananchi kupata habari.
Wadau mbalimbali wa habari wakiwemo chama cha wamiliki wa vyombo vya habari MOAT wamekuwa wakilalamikia maudhui ya muswada huo kwa madai ya kuminya uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki ya kupata taarifa kwa wananchi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni