.

.

08 Mei 2016

WASIKIE CANAVARO, MSUVA WALIVYOFUNGUKA KUHUSU USHINDI WA JANA


NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro' ameweka wazi siri za ushindi wa mabao 2-0 dhidi GD Sagrada Esperanca ya Angola ulitokana na kujituma, kutumia nguvu pamoja na kufuata maelekezo ya kocha wao.

Akizungumza na CHAMBUZI NEWS, Canavaro alisema "Sisi tunataka  kuweka historia Afrika Mashariki  kwa kuwa moja ya timu itakayofanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa na tuna timu nzuri pia."

Canavaro alisema kuwa endapo wangekuwa makini zaidi hasa safu ya ushambuliaji basi timu hiyo ingepata magoli zaidi ya hayo.

"Kwa sasa akili zetu zipo kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa Mei 17 huko kwao Angola, itakuwa mechi ngumu ila tutapambana ili tuweze kufuzu hatua ya makundi,'' alisema Canavaro.

Wakati huo huo, mfungaji wa bao la kwanza la Yanga, Simon Msuva alisema:''Timu yetu ilijiandaa vizuri na ndiyo maana tumefanya vizuri, nilijituma mazoezini huku nikijijenga kisaikolojia.''

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni