.

.

08 Juni 2015

SWEDEN NA TANZANIA KUKUZA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA


Mbeyafm Redio's photo.
NCHI ya Sweden imedhamiria kuukuza ushirikiano wake na Tanzania kwa Awamu mpya ambayo itaongeza uwekezaji na biashara zaidi.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Muungano wa wafanyabiashara wa Sweden, Business Sweden, Ylva Berg alimueleza Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wake na Rais Kikwete juzi katika Kituo cha Biashara jijini Stockholm.
"Tunataka kushirikiana, kufanya biashara na uwekezaji na Tanzania hapa kwenye masuala ya nishati" alisema Berg. Sweden inachangia Dola za Marekani bilioni 1 katika Mfuko wa Nishati wa Rais Barack Obama wa Marekani maarufu kama Power Africa, ambao unalenga katika kuongeza idadi ya watu wanaotumia umeme barani Afrika.
Mpango huo unaanza kwa nchi 6 ambazo ni Tanzania, Ethiopia, Ghana, Liberia, Kenya na Nigeria. Katika mkutano huo Rais Kikwete amewaeleza wafanyabiashara hao ambao pia ni wamiliki wa makampuni makubwa ya kimataifa kuwa Sekta ya Nishati ni sekta inayokua kwa haraka sana nchini Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni