Akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu
ambao asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji Mh lowasa amesema pamoja na
azima yake ya kutoa elimu bure mashuleni pia itakuwa bora yenye
mafanikio yanayoonekaana kwa vitendo kwa wananchi wengine.
Aidha Mh Lowassa amesema elimu ikitumika viziri na watu wote
wakaelimika umaskini utapungua na pia unyanyasaji wa watu wa kipato cha
chini utapungua.
Waziri mkuu wa awamu ya tatu Mh Fredrik Sumaye amesema asilimia
kubwa ya matatizo yanayowakabili wakulima na wafugaji wakiwemo wa mkoa
wa Simiyu ni matokeo ya kukosa misingi imara inayo changiwa na mfumo
mbaya wa elimu na ndio maana UKAWA imeweka msukumi mkubwa katika elimu
kama wananchi wakiichagua kuingia madarakani.
Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Bw Godwin Samba amewaomba
wananchi wa Bariadi wamchague yeye na viongozi wengine wa UKAWA ili
wamalize matatizo sugu yanayo wakabili wakulima na wafugaji kwa muda
mrefu sasa.
Mh Lowassa ambaye amefanya mikutano katika maeneo mbalimbali ya
mkoa wa Simiyu anaendelea kunadi sera ya mabadiliko katika mkoa wa
Kagera.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni