.

.

14 Septemba 2015

MASHABIKI WA SOKA WAWAKATAA WAKIMBIZI


Wakati dunia ikiendelea kusikitishwa na kitendo cha wahamiaji ambao wamekua wakiingia kwenye nchi za barani Ulaya kutokana na machafuko yanayoendelea kukithiri katika nchi zao, mashabiki wa klabu ya Maccabi Tel Aviv ya nchini Israel wameonyesha kuwa tofauti.
Wakati wa mchezo wa ligi ya nchini humo ukichezwa mwishoni mwa juma lililopita, mashabiki wa klabu hiyo walionyesha bango lililokua likipinga nchi yao kuwapokea wakimbizi kutoka kwenye nchi yoyote duniani.
Mashabiki walilionyesha bado hilo bila uoga na walidhamiria kufanya hivyo kutokana na kuamini kwamba nchi yao haina mantiki yoyote ya kuwa na watu watakaopokelewa kama wakimbizi, kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani hususan za barani Ulaya.
Kwa lugha ya kiingereza bango hilo lililosema ‘Refugees Not Welcome’ hali ambayo ilionekana kuwasikitisha waandishi wa habari kutoka nje ya nchi ya Israel ambao walikua wakifuatilia mchezo wa Macabi Tel Aviv dhidi ya Kiryat Shmona ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.
Waandishi hao wa habari walionyesha hasira zao kwa kupiga picha kitendo hicho na kuzianika katika mitandao mbali mbali ya kijamii pamoja na habari kwa kuonyesha ni vipi baadhi ya watu wa Israeli walivyoonyesha kuwa kinyume na wengine duniani.
Hata hivyo waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameshatoa amri ya kujengwa kwa uzio katika mipaka ya nchi hiyo ili kuzuia wimbi zaidi la wakimbizi ambao wamedhamiria kukimbilia nchini kwake.
Lakini hali ilionekana kuwa tofauti kwa mashabiki wa soka nchini England, hususan wa klabu za Arsenal pamoja na Everton, ambapo mwishoni mwa juma lililopita wakati wa michezo ya ligi, walionyesha mabango ya kuishinikiza serikali yao kuendelea kuwapokea wakimbizi kutoka katika nchi mbali mbali duniani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni