.

.

14 Februari 2016

KUELEKEA MCHEZO KATI YA ARSENAL VS LEICESTER LEO






Arsenal haina majeruhi mpya kuelekea mchezo wa Jumapili dhidi ya Kinara wa ligi hiyo Leicester City katika uwanja wa Emirate. Francis Coquelin yuko katika hali nzuri kuweza kutajwa kikosini ilhali Danny Welbeck akitarajiwa kujumuishwa kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya majeraha ya mguu kwa muda mrefu.
Leicester inatarajiwa kutokubadilika kabisa huku ingizo jipya la mwezi Januari Daniel Amartey akiwa hayuko bado katika mafikirio ya kucheza akiwa katika mpango wa kujiimarisha kimwili.
Kwa upande wa wale waliokuwa nje kwa muda mrefu Jeff Schlupp na Matty James wenyewe bado kurejea dimbani.
Mchambuzi John Motson katika uchambuzi wake anasema nafasi kubwa ya juu kuwahi kushikwa na Leicester ilikuwa ni katika msimu wa 1928-29 ambapo walimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Sheffield Wednesday.
“Wanaendelea kushika nafasi nzuri hadi sasa kiasi kuakisi msimu wa 1928-29. Kwasasa wakiwa wamefungwa michezo mitatu katika michezo 34 ukianzia na ligi iliyopita jumlisha ma michezo ya ligi msimu huu.
“Baadaa ya mchezo wa kesho uwanja wa Emirates, Leicester City watakuwa na michezo miwili tu dhidi ya timu zilizo katika nafasi sita za juu katika ligi ambapo ushindi wa kesho ni kwamba utakuwa ukiongeza matumaini ya kushinda ligi.
“Ratiba ya mchezo huo wa Jumapili pia ina maana sana kwa Arsenal kujaribu kujenga ushawishi wa kutwaa taji kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12.
“wikiendi iliyopita Arsenal ilimaliza njaa ya ushindi ya michezo minne mfululizo na bila shaka hawatataka kurejea katika mtirirko huo mbaya wa matokeo kama wanataka kukimbiza ubingwa.
Historia walipokutana.
Arsenal ilishinda mchezo wa mwezi Septemba mwaka jana 5-2, kikiwa ni moja kati ya vipigo viwili vya Leicester msimu huu.
Ndiyo timu pekee ambayo inaweza kumaliza ligi ikiwa washindi mara mbili dhidi ya Leicester msimu huu wa 2015-16.
Leicester haijawahi kuifunga Arsenal katika michezo 18 iliyopita waliyokutana(D6, L12).
Mchezo wa mwisho Leicester kuifunga Arsenal ulikuwa Novemba 1994 katika ligi Leicester wakiwa katika uwanja wa nyumbani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni