.

.

12 Januari 2016

NIGHT INSPIRATION YAFANA KATIKA UKUMBI WA TUMANYENE SOCIAL HALL.


 Mkurugenzi wa EGYBUSINESSSOLUTION‬ ndg Elly Bonke akizungumza na wananchi katika ukumbi wa Tamanyene Social Hall.

 Mkurugenzi wa EGYBUSINESSSOLUTION‬ ndg Elly Bonke akizungumza jambo.

                                                 Washiriki katika picha ya pamoja.
 
               Washiriki wakimsikiliza jambo kwa mmoja wakiongozi wa EGYBUSINESSSOLUTION‬ 




Watu mbalimbali waliodhuria ukumbi wa Tumanyene Social Hall wakipata chakula cha pamoja.
Meza kuu wakipata chakula kwa pamoj.


Usiku wa matumaini wafana katika ukumbi wa Tumanyene Social hall,ulipo nzonvwe jiji Mbeya ambapo kauli mbiu yake ilikuwa FUKUZIA NDOTO ZAKO ,na huwa inafanyika kila tarehe ya mwisho wa mwaka,kwa mwaka jana haikuweza kufanyika kufuatana na mambo kuingiliana hivyo kuweza  kufanyika usiku wa tarehe 10/01/2016.
 Katika mambo ambayo yaliweza kuzungumzwa ni pamoja na kujitambua pamoja na kutimiza malengo kwa yale mambo ambayo unayafikilia na kutamani mafanikio ya wale watu waliofanikiwa ili nawe tu uweze kutimiza malengo ,moja ya vitu nikama kujiamini kufanya kitu hata kama umesoma,kutokata tama katika maisha pamoja na malengo uliyojiwekea.
Nae mmoja wa waandaaji wa shughuli hii Ndg Elly Bonke ambaye ni mkurungezi wa kampuni ya EGGY BUSINESS SOLUTION aliweza kuzungumza na watu mbalimbali waliofika nakuwasii kutokata tamaa na chochote kile katika maisha endapo tu utakuwa na nia ya kufanya hicho kitu pamoja nakuonesha mifano mbalimbali kwa watu waliofanikiwa na hawakuweza kukata tama.
Katika upande wa muwezeshaji wa shughuli hiyo Mchungaji Aliko Mwalulili aliweza kuzungumza na wananchi waliodhuria katika ukumbi wa Tumanyene Social hall na kuwataka wasikate tama na wamtegee mungu kwa kila jambo pamoja na kuwasii kuwa kitu kidogo ambacho unaweza kukipata waweza kukiwekea malengo na ukafanyia kitu kikubwa katika upande wa biashara huku nae akionesha mifano mbalimbali kwa watu waliofanikiwa kufuatana na kile kidogo walichokipata na sasa nikikubwa kwao kufuatana na faida walizozipata pamoja na kuondoka katika hali ya umasiki.

Picha zote na Chambuzi News
  



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni