.

.

01 Aprili 2016

MADIWANI WILAYANI KYELA WAMEITISHA KIKAO CHA BARAZA LA DHARULA KUJADILI JINSI ALIVYOKAMATWA DIWANI MWENZAO.

Na Msuli Mwaijengo-kyela Mbeya

MADIWANI wilayani Kyela Mbeya,wameitisha kikao cha baraza la dharula kujadili jinsi alivyokamatwa diwani mwenzao kutoka kata ya Lusungo,Veronika Kanyanyila wakidai mkuu wa wilaya hakutenda haki.
Diwani wa kata hiyo,Veronika Kanyanyila alikamatwa juzi na na kutupwa lumande na mkuu wa wilaya hiyo,Dr,Thea Ntara kwa madai kuwa anakwamisha zoezi la kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu ilioikumba wialaya hiyo.
Kutokana na hali hiyo,madiwani kwa pamoja bila kujali itikadi za vyma vyao,walimuandikia barua mwenyekiti wa halmashauri hiyo kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri Clement Kasongo aitishe baraza la dharula kujasdili suala hilo.
Kupitia baraza hilo,mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Dr,Hunter Mwakifuna ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani humo, aliitisha baraza hilo na kusoma barua aliyoandikiwa na mkurugenzi wa halmashauri akiomba kuhairishwa kwa kikao hicho.
Kufuatia kauli hiyo ya mkurugenzi kuahirisha kikao hicho kiliwachefua madiwani hao ambao walimtuhumu mkurugenzi kwa kukaidi agizo hilo ambapo walimtaka mwenyekiti huyo aende mkoani Mbeya kuonana na mkuu wa mkoa.
Athumani Sampa (CCM) diwani kata ya Ibanda,na Paul Mwambafula wa Bujonde walisema kitendo cha mkuu wa wilaya kumuweka lumande diwani mwenzao ni udharirishaji ambapo alisema hakufuata kanuni na sheria za utawala bora na kumtaka aombe radhi.
:Ndugu mwenyekiti,baraza hili alimjadili mkuu wa wilaya,tunajadiri jinsi madiwani tunavyonyanyashwa,tunaomba upeleke kilio hiki kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala tufanye nae kikao vinginevyo hatutaweza kufanya kazi za wananchi kwa kuhofu kuwekwa ndani na mkuu wa wilaya.
Claud Fungo diwani wa mbugani,Victoria Ipopo viti maalum (CHADEMA) walisema haoni sababu ya kushirikiana na mkuu huyo wa wilaya kwa kuwa ametumia udikteta,ubabe hivyo wamemtaka mwenyekiti kupeleka kwa maandishi malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa
Diwani wa kata ya Lusungo,Veronika Kanyanyila,aliyewekwa lumande na mkuu wa wilaya,alisema kitendo alichofanyiwa na mkuu wa wilaya ni cha kiuonevu kwani kama alimkosea ilipaswa apelike amshitaki kwenye kamati ya maadiri na si kumkamata kama kuku.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Dr,Hunter Mwakifuna alikiri kuandikiwa barua na madiwani hao wakitaka kuitishwa kwa kikao cha dharula kujadili sababu za kukamatwa kwa diwani mwenzao na kusema kuwa leo anaenda kwa mkuu wa mkoa kupeleka malalamiko hayo.
Dr,Mwakifuna aliwasihi madiwani hao kufanya kazi za kuwatumikia wananchi kwa kuwa ndiyo waliowachagua na kwamba ataongozana na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo hadi kwa mkuu wa mkoa na kuleta mrejesho katika kikao kijachao,ambapo alilaani vikali kukamatwa kwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni