Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF) Ernest Sungura
amesema taasisi yake iko tayari kugharamia matangazo ya Bunge kupitia
TBC ikiwa suala ni ukosefu wa fedha.
Amezungumza hivi
sasa kwenye mkutano na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari nchini
mbele ya Mkurugenzi wa Maelezo Assah Mwambene na Balozi wa Ireland.
Amesema kwamba lengo la TMF ni kuleta mabadiliko katika tasnia ya habari na kuona wananchi wanapata taarifa.
Awali Bw.
Mwambene amesema kwamba serikali watafikiria kupeleka maombi TMF kuomba
uwezeshwaji katika maandalizi ya miswada miwili ya sheria za habari ili
kupitisha sheria zenye matakwa ya wadau.
Kuhusu hilo,
Sungura amesema taasisi yake iko tayari kuisaidia serikali kwenye
mchakato huo na hata kuitisha kongamano kubwa la wadau.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni