Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa
uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani
uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo
kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified". Mjema alizindua uwanja huo leo
katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate
akishuhudia tukio hilo.PICHA NA MICHUZI JR
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa
shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto)
akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia
kampeni yake ya "Be Kidotified" uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa
pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara
Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule
Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Mrembo
wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi
katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli
uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo.
Mandhari
ya uwanja wa Mpira wa Kikapu na Netiboli wa shule ya Sekondari ya
Jangwani uliojengwa na Mrembo, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya
"Be Kidotified".
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye hafla
fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya
Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya
Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Kidoti, Jokate Mwegelo.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema kuwa
amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji
Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.
Mjema
alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata
shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya "Be Kidotified". Alisema kuwa
amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na
kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya
kuendeleza michezo na taaluma.
Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi milioni 50.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo vitamwezesha mshiriki kupata ajira.
Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi kuonyesha vipaji vyao ipasavyo.
Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo, lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi.
“Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ”
“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation, na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate.
Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu.
Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila siku.
MECHI NYINGINE ZA KUJIPIMA NGUVU ZA AZAM FC HIZI HAPA
KLABU
Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, leo asubuhi imeanza tena
mazoezi yake baada ya mapumziko ya jana huku ikitarajia kucheza mechi
mbili za kirafiki kwa mujibu wa programu ya wiki hii.
Azam
FC ilipumzika jana Jumatatu ili kuondoa uchovu wa kambi ya Zanzibar,
ambayo ilikuwa ni sehemu ya muendelezo wa maandalizi ya msimu ujao
unaotarajia kuanza Agosti 17, mwaka huu kwa kucheza mchezo wa Ngao ya
Hisani dhidi ya Yanga.
Mabingwa
hao katika programu ya wiki hii wataendelea kucheza mechi za kirafiki,
ambapo kesho Jumatano saa 10.00 jioni itacheza na JKT Ruvu kwenye Uwanja
wa Azam Complex.
Mbali
na mchezo huo, Jumamosi ijayo itakipiga na Ruvu Shooting nyumbani kwao
kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani, mechi ambayo itafunga maandalizi ya
Azam FC wiki hii kabla ya kupumzika Jumapili ijayo.
Mpaka
sasa Azam FC imeshacheza mechi tano za kirafiki zote ikishinda kwa
kuzilaza, Friends Rangers (2-1), Ashanti United (1-0), Mshikamano (1-0),
Wilaya ya Mjini (1-0) na Taifa ya Jang’ombe (1-0).
Kikosi
hicho kinakaribia kufikisha mwezi sasa tokea kilipoanza kufundishwa na
makocha wapya kutoka Hispania, Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi
wake, Yeray Romero, Kocha Mkuu wa Viungo, Jonas Garcia, Msaidizi wake,
Pablo Borges, Kocha wa Makipa, Jose Garcia na Mtaalamu wa Viungo, Sergio
Perez Soto.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni