Kikosi cha Mbeya City Fc tayari kipo jijini Tanga kwa ajili ya
mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya African Sports
unaotajia kuchezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mapema leo mkuu wa kitengo cha utabibu kikosi Dr Joshua Kaseko
amesibitisha kuwa wachezaji wote 18 walisafiri kutoka jijini Mbeya tayari
wa mchezo huo wako kwenye hali nzuri kabisa na ana imani kubwa watacheza kwenye
kiwango bora ili kuipatia matokeo timu yao hapo kesho.
“Joseph Mahundi alipata majeraha kwenye
mchezo uliopita, hivi sasa yuko vizuri na tunatarajia atakuwa sehemu ya
kikosi hapo kesho, hakuna shaka kuwa City iko hapa Tanga kwa
sababu ya kupata matokeo na hakuna jambo lingine, tumetoka
kushinda dhidi ya Stand United jambo linalotupa nguvu ya
kupambana hapo kesho, tuna morali ya hali ya juu kikosini ambapo kila
mmoja ana hamu ya kurudi na pointi tatu” alisema.
Kwa upande wake Kocha Kinnah Phiri ameweka wazi kuwa japo hali ya
hewa ya hapa ni tofauti kabisa na ile iliyopo jijini Mbeya lakini hiyo siyo
sababu ya City kukosa ushindi hapo kesho
“Hali ya hewa ya hapa ni tofauti sana na
iliyopo jijini Mbeya, hilo hatulitizami sana, tumejiandaa vya kutosha, asubuhi
ya leo tumemaliza mazoezi na wachezaji wamepewa muda wa kuweka miili yao sawa
kwa kwenye barafu, hakuna shaka yeyote kuwa tunazo pointi tatu kutoka
hapa” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni