NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jaffo akikagua Vyoo kaktika Soko la Mwanjelwa. (Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mwonekano wa Soko Jipya la Mwajelwa. |
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi) Suleiman Jaffo, ameiagiza halmashauri ya Jiji la Mbeya,
kuhakikisha inaliimarisha soko jipya na la kisasa la Mwanjelwa ili liwe kivutio
kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.
Amesema,
endapo soko hilo litaenda vizuri, watu wote kutoka nchi mbalimbali hususani
nchi za kusini mwa afrika, watakuwa wanaishia hapo na kuendesha shughuli zao.
Jaffo,
aliyasema hayo juzi wakati akitembelea na kukagua Soko hilo la Mwanjelwa ambalo
ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 20 zilizotolewa kwa mkopo
kutoka benki ya CRDB.
Amesema,
kama viongozi watakuwa na mikakati madhubuti na yenye tija samabamba na
kutanguliza uzalendo, Soko hilo litakuwa ni kitovu cha biashara, na ndani ya
miaka mitano kunawatu watakuja kujifunza hapo.
“Hivi
karibuni nilibahatika kusimamia uchaguzi wan chi za nje kama mbili hivi,
Zimbabwe na Zambia lakini nilijionea wafanyabiashara wa hapo wakiendesha
shughuli zao kwa kutumia malighafi kutoka Tanzania tena kutoka Soko la
Kariakoo,”amesema.
Amesema,
hivyo kama viongozi watajipanga vizuri, watakuwa wameiweka nchi kwenye nafasi
nzuri ya kibiashara na nchi kuwa miongoni mwa Taifa linaloenda kwa kasi
kiuchumi.
“Hakuna
miujiza kwa hili, jambo la msingi ni watu kuwa wazalendo, kutumia vizuri
rasilimali tulizokuwa nazo tena kwa uadilifu mkubwa,”alisema.credit Fahari News
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni