.

.

03 Aprili 2016

MADIWANI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA WAKUBALIANA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KILA MWISHO WA WIKI.

Madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilayani kyela wamekubaliana kufanya usafi wa mazingira kila mwisho wa wiki ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania John pombe magufuli kufanya usafi kila mwisho wa mwezi.
Mratibu wa zoezi hilo ambaye ni diwani wa kata ya mbugani Claud Fungo amesema wameamua kuunga mkono kauli ya hapa kazi tu kwa vitendo tofauti na baadhi ya viongozi wa serikali kushindwa kufanya kazi na kubaki kuwasimamia wananchi .
Kwaupande wake diwani wa kata ya mikoroshoni Bruno sanga na madiwani kutoka katika kata za nkuyu na itunge wamesema kujikitokeza kwao kufanya usafi wa mazingira kutawahamasisha wananchi kufanya shughuli za maendeleo pamoja na kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa ukiibuka mara kwa mara wilayani hapa.Naye mwenyekiti wa kitongoji cha butiama Anton Mapunda ameamua kuungana na zoezi hilo linaloendeshwa na madiwani wa chadema kwa kuwa yeye ni muumini wa maendeleo na kutoa wito kwa viongozi wengine kujitoa ili kufanya waliyowaahidi wananchi.Zoezi la kufanya usafi kila mwisho wa wiki ambalo litafanywa na madiwani wa chadema litafanyika kwa kila kata iliyopo wilayani hapa ikiwa ni pamoja na kufanya usafi mashuleni,katika vituo vya afya na zahanati ili kuhakikisha kyela inakuwa safi na kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kinachosababishwa na uchafu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni