.

.

03 Aprili 2016

WATU 17 WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA WAKAMATWA KWA KUTOKUWA NA VYOO.


Watu 17 wakazi wa Kijiji cha Lusungo Kata ya Lusungo Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya wamekamatwa kwa kutokuwa na vyoo na uchafu wa mazingira hivyo kuzorotesha juhudi za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu Wilayani kyela.
Ugonjwa huo umedumu kwa kipindi cha miezi mitatu sasa na Kata ya Lusungo na Ndobo ndizo pekee bado zina wagonjwa wa kipindupindu hali iliyomfanya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Dakta Thea Ntara kupiga kambi Kata ya Lusungo ili kufanya ukaguzi wa vyoo na usafi wa mazingira.
Katika mchakato huo maalumu uliofanywa na Mkuu wa Wilaya aliyeambatana na Maafisa wa Afya pia uliyakumba maeneo mbalimbali kama Kata ya Ikama na Kijiji cha Tenende ambapo alilazimika kuvunja Kilabu cha pombe Kata ya Ikama baada ya kuwakuta wakazi wa eneo hilo wakinywa pombe za kienyeji katika mazingira machafu.
Kwa upande wake Afisa Afya Geophrey Baroshi amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na watahakikisha kila kaya ina choo na kuwa na mazingira safi kwa muda wote ili kuutokomeza kabisa ugonjwa huo Wilayani Kyela na kwamba waliokamatwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.Mtendaji wa Kijiji cha Lusungo Fadhili Sade na Mtendaji wa Kata ya Lusungo Stephen John wamesema kuwa mpaka sas wamefanya ukaguzi katika kaya 681.na wwameahidi kupamaba navyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni