Katika kuunga mkono jitihada za Rais
Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi
kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk.
Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga
na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa
madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika wilaya
hizo.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi pesa
hizo kwa wakuu wa wilaya wa kampuni hizo, Dk. Mengi alisema ni muhimu
kwa watanzania kuungana kwa pamoja na kusaidia kupatikana kwa madawati
kwani kwa kufanya hivyo ni kulisaidia taifa.
Hata hivyo Dk. Mengi alisema kuwa anaamini
kama watu matajiri nchini wakiungana kwa pamoja na kujadili jinsi ya
kumaliza tatizo la madawati nchini basi jambo hilo litaweza kupatiwa
ufumbuzi wa haraka tofauti na sasa ambapo linakwenda kwa mwendo wa
kusuasua.
"Ukisaidia mtu mmoja katika elimu ni sawa
umesaidia jamii na taifa kwa ujumla kama watu matajiri wakisema wakae
kwa pamoja na kuangalia jinsi ya kumaliza tatizo hili linaweza
kutatuliwa na shida ya madawati kumalizika.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP,
Dk. Reginald Mengi akizungumza katika halfa ya kukabidhi milioni 70 kwa
wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo zitawezesha wilaya hizo kununua
madawati 1,000 na kila wilaya kupata madawti 500.
"Matajiri wanatakiwa kutambua kuwa
wanatakiwa kurudisha shukrani zao kwa Mungu, taifa na wananchi na hasa
kwa walio na hali ya chini kwani hao ndiyo wanaowasaidia kufanya
biashara zao kwa amani," alisema Dk. Mengi.
Aidha amewataka wakuu wa wilaya hizo
kuondoa hofu ya kufukuzwa kazi kama watakuwa hawajakamilisha na
wanachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuongeza juhudi huku akiwashauri
kuandaa mikutano katika wilaya zao na kushirikisha wananchi wao ili
waweze kuchangia na hatimaye tatizo hilo kumalizika.
Kwa upande wa mkuu w wilaya ya Bagamoyo,
Alhaj Majid Mwanga na mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab
wamemshukuru Dk. Mengi kwa msaada ambao amewapatia na kuwataka
watanzania wengine kuwa na moyo wa kujitolea kama jinsi amevyofanya Dk.
Mengi kwa kuchangia upatikanaji wa elimu bora.
Awali kabla ya msaada ambao umetolewa na
Dk. Mengi, wilaya ya Bagamoyo ilikuwa ikikabiliwa na upungufu wa
madawati 2,463 na Handeni ikikabiliwa na tatizo la upungufu wa madawati
4,000.
Mkuu wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab akizungumza katika halfa hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid
Mwanga akizungumza katika halfa ya kupokea pesa kwa ajili ya madawati
500 yatakayokwenda katika wilaya yake kusaidia kupunguza tatizo la
madawati.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akisaini mfano wa hundi kabla ya kuanza kuwakabidhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP,
Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35, Mkuu wa
wilaya ya Haneni, Husna Rajab. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mji wa
Handeni, Kenneeth Haule, Mwenyekiti wa Mji wa Handeni, Twaha Mgaya na
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Handeni, Ramadhani Diliwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP,
Dk. Reginald Mengi akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni 35 kwa ajili ya
ununuzi wa madawati 500, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid
Mwanga. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Chalinze, Edes Lukoa, Mkurugenzi
wa Bagamoyo, Natujwa Melau, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally
Issa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Said Zikatimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni