Watu 46
wameripotiwa kuuawa ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya mwanzoni mwa
mwaka huu katika ghasia zinazoendelea nchini Burundi.
Wizara ya
Usalama wa Uma nchini Burundi imetangaza kuendelea machafuko ambapo watu
46 wameuawa tokea mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016 pekee. Kwa mujibu wa
wizara hiyo katika machafuko hayo, watu wengine 215 wamejeruhiwa.
Hata hivyo
Alain-Guillaume Bunyoni Waziri wa Usalama wa Uma nchini humo ameongeza
kuwa, hali ya mambo imeboreka kidogo mwezi huu wa April ikilinganiswa na
miezi iliyopita.
Amewatuhumu
wapinzani wa serikali kuwa waroho wa madaraka na kuwahusisha na
machafuko hayo yenye lengo la kuharibu usalama wa taifa hilo. Mwaka
mmoja umetimia tangu Burundi itumbukie katika hali ya mchafukoge mwezi
Aprili mwaka jana, kufuatia hatua ya chama tawala cha CNDD-FDD
kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza kugombea tena urais katika uchaguzi
uliopita nchini humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni