.

.

14 Mei 2016

UVIMBE UNAOTAJWA KUTOKANA NA MARADHI YA SARATANI WAMSUMBUA MTOTO CHRISTINA.

Huyu ni mtoto Christina Nduta Mbomba (4) (Pichani) mkazi wa Nzovwe jijini Mbeya ambaye amepatwa na uvimbe ambao unatajwa kutokana na maradhi ya saratani.
Kwa mujibu wa maelezo ya mama wa mtoto huyu, Mariam Wailes ni kuwa tatizo la mtoto lilianza kama mtoto wa jicho katika jicho lake la kushoto katika hospitali ya Rufaa,Mbeya mwaka jana 2015, mwezi 8 na akapata tiba lakini hali ikawa mbaya zaidi na kusababisha mtoto kutolewa jicho mwezi disemba 2015 zoezi ambalo lilifanyika katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam na kugharimu jumla ya Tsh. 150,000,0.
Baadae mwaka huu mwezi machi alianza kutokwa na uvimbe katika mahala lilipotolewa jicho ambapo suluhu inatakiwa mtoto huyu apelekwe hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Kinachoombwa kwako ni msaada wa hali na mali ili kuiwezesha familia hii kumpeleka mtoto kupata tiba kwakuwa wazazi wa mtoto wamedai kutokuwa na uwezo wa kumtibia mtoto Christina kwa sasa.
Unaweza kumchangia kwa M-Pesa namba 0763260481 au kupata maelezo zaidi juu ya tatizo hilo. Jina lililosajiliwa ni Nduta Mboma.


VIDEO MAMA MZAZI WA CHRISTINA AKIZUNGUMZA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni