.

.

10 Mei 2016

WANAKOMA KUMWANYA WAKUBALI KICHAPO CHA GOLI 2 KWA 0 DHIDI YA YANGA SC.


Mpira umemalizika katika uwanja wa kumbukumbu wa sokoine mkoani Mbeya,huku Yanga Sc ikiibuka na ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Timu ya Mbeya city Fc,ambapo magoli yalipatikana kupitia kwa Vincent Bossou mnamo dakika ya kumi na 16 ya mchezo kipindi cha kwanza huku timu zote mbili zikijaribu kushambuliana kwa wakati tofauti tofauti, dakika ya 20 hadi 22 ya mchezo mbeya city walionekana kumiliki mpira  zaidi katikati ya uwanja,mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Yanga walikuwa mbele kwa goli 1 kwa sifuri,Dk 53 hadi 54, Yanga bado walionekana kumiliki mpira vizuri hasa eneo la katikati
Dakika 50, Msuva alijaribukupiga shuti kali kabisa. Lakini Kasejaaliokoa kwa umakini mkubwa,Dakika 88, Ngoma alipokea pasi nzuri ya Tambwe, lakini alipiga  shuti kuuuubwa na mpira huo kutoka nje.
Dakika 85 Amis Tambwe aliweza kuwainua mashabiki wa yanga na kupiga shuti kali na kuiyandikia Yanga SC goli la pili,mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa Yanga Sc 2 Mbeya city fc 0,na kufanya timu ya Yanga kufikisha pointi 71wakishilia ligi kuu Tanzania Bara msimu wa Mwaka 2015/2016 huku mbeya city fc wakiwa katika nafasi ya nane na pointi 33,Mbeya city fc amebakiwa na michezo miwili Mwadui mjini Shinyanga na Ndanda uwanja wa Sokoine Mbeya,Huku Yanga akibakiwa na michezo miwili kati ya Ndanda Fc utakao chenzwa uwanja wa taifa Dar es Salaam tarehe 15 mwezi huu na mechi ya mwisho atacheza na Majimaji Songea.












Hakuna maoni:

Chapisha Maoni