Kumekuwepo na imani kuwa wasanii wengi wanaogopa kumshirikisha Lady
Jaydee kwasababu wanaamini Clouds FM haitoishia tu kutoucheza wimbo huo
bali hata zingine zijazo.
Clouds FM na Lady Jaydee wana tofauti ambazo hadi sasa hazijamalizika.
Muimbaji huyo wa Ndindindi amefanikiwa kuelezea suala hilo kupitia kituo
cha redio cha Nyemo FM cha mjini Dodoma alikoenda kwaajili ya show yake
iliyofana ya Naamka Tena Concert.
“Inawezekana pia lakini hawawezi kusema labda moja kwa moja,” Jide alimjibu mtangazaji wa redio hiyo, Winston Makangale.
“Lakini pia sio vizuri umwongelee mtu ambaye hujui mawazo yake
yanafikiria nini au pengine unaweza ukaongea hivyo halafu ikawa sio
hivyo ukawa umemsingizia,” aliongeza.
“Kwahiyo nafikiri hilo tuwaachie wao kila mmoja atakuwa anajua kwa nafsi
yake kama anaweza au hawezi na sababu zipi zinazopelekea aweze na
sababu zipi zinazopelekea asiweze. Lakini la msingi kila mmoja afanye
muziki wake kwa nafasi yake na watu waweze kuburudika.”
“Mimi sina tatizo na mtu yeyote ambaye atakuwa yupo tayari kufanya kazi
na mimi,” Jaydee alijibu baada ya mtangazaji kusema anatamani kusikia
collabo yake na Diamond.
“Bado hatujakutana na wala hatujawahi kukaa kuzungumzia kuhusiana na collabo.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni