.

.

11 Juni 2016

RAIS AMTEUA MWIGULU KUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI.

Mbeyafm Redio's photo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo amemteua Mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri walioteuliwa katika mabadiliko haya wataapishwa Jumatatu tarehe 13 Juni, 2016 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni