.

.

14 Juni 2016

TMF YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI NCHINI KUKIMBIZANA NA TEKNOLOJIA.

MKUREGENZI WA MFUKO WA KUSAIDIA VYOMBO VYA HABARI NCHINI (TMF) ERNEST SUNGURA ALIYESIMAMA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA UKUMBI WA FLOMI MJINI MOROGORO.

MOROGORO
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuendelea kujifunza uandishi wa kisasa unaotumia kasi ya Teknolojia na kuacha kuandika kwa mazoea kwa kutumia mbinu za kizamani.

Wito huo umetolewa leo mjini Morogoro na mkurugenzi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini Ernest Sungura wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya awali kwa waandishi wa habari waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari za vijijini.

Sungura amesema kuwa taaluma ya uandishi wa habari kwa sasa inahitaji waandishi wanaopenda kujifunza mara kwa mara kwani maendeleo ya matumizi ya teknolojia kila siku yanabadirika.

Sambamba na hayo Sungura ameongeza kuwa mwandishi ambaye hapendi kujifunza na akaendelea na uandishi wa habari wa kizamani atakosa soko la ajira katika ulimwengu wa sasa unaokimbizana na teknolojia ya mitandao.

Katika hatua nyingine amewataka waandishi wa habari waliopata ruzuku ya kuandika habari za vijijini kuzitumia pesa hizo za ruzuku katika malengo yaliyokusudiwa ili kufanikisha kufikia malengo ya kusaidia jamii hususan za vijijini.

Kwa upande wake Afisa miradi wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini  Dastani Kamanzi amewataka waandishi wa habari kuandika habari zenye ukweli pasipo kupendelea upande wowote.

Mafunzo ya awali ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Flomi mjini Morogoro yameshirikisha waandishi wa habari thelathini waliofanikiwa kupata ruzuku ya kuandika habari za vijijini kati ya waandishi miamoja arobaini na sita waliomba nchi nzima.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni