jana tarehe 30/03/2015 waandishi wa habari walifika kituo Kikuu
cha Polisi wakitaka kujua uhalali wa silaha iliyokamatwa tarehe
29/03/2015. Silaha hiyo ni Bastola aina ya BERRETA yenye
namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu. Pia zilikamatwa risasi 17 za
Ufafanuzu ni kama ifuatavyo:
Uchunguzi wa kina na wa kitaalam sasa umethibitisha kwamba
silaha hiyo inamilikiwa kihalali na Askofu Josephat Gwajima.
Kuhusu risasi 17 za Short Gun ni kwamba Askofu Gwajima
anamiliki Bunduki aina ya Short Gun yenye namba 102837
ambayo inatumia risasi za aina ya hizo zilizokamatwa.
Kuhusu watu 15 wanaotuhumiwa kujaribu kumtorosha Askofu
Josephat Gwajima bado uchunguzi unaendelea. Aidha watu hao
pia wanahojiwa kuhusu suala la kukutwa na silaha na risasi
zilizotajwa hapo juu wakati wao sio wamiliki halali za silaha hiyo
na risasi hizo na idadi iliyotajwa kwa mujibu wa sheria.
Baada ya uchunguzi wa suala hilo jalada la kesi litapelekwa kwa
mwanasheria wa Serikali kabla hawajafikishwa mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake.
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
S. H. KOVA,
DAR ES SALAAM.
Tupe Maoni Yako( Usiandike Matusi )
Sakata la mwanafunzi
aliyekutwa amekufa ndani ya shimo la majitaka limechukua sura mpya baada
ya wananchi wenye hasira kali kuchukua sheria mkononi baada kuvunja na
kuichoma moto nyumba.
Tazama ilivyo anzwa kuchomwa moto
Tatizo la kujichukulia Sheria mkononi limeendelea kuwa kubwa kwa jamii
ya watanzania, katika sakata la hivi karibuni ambapo baadhi ya watu
walikuvunja na kuichoma moto nyumba ya mkazi mmoja wa mtaa mbwile b
jijini Mbeya kwa tuhuma za kubaka na kumuua mwanafunzi wa miaka nane.
Nyumba ikiwa imebomolewa
Katika hali isiyo ya wakawaida wakazi hao wamejikuta wakichukua sheria
mkononi kwa kuivunja na kuichoma moto nyumba ya Mariamu kasonta baada
ya kumtuhumu mlinzi wake kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili katika
shule ya msingi majengo mwenye umri wa miaka nane jina limehifadhiwa na
kisha kumkuta akiwa ameuwawa na kutupwa katika shimo la maji taka.
Wakazi hao ambao walipimga vibaya mlinzi huyo aliejulikana kwa jina moja
la Charles ambae alikamata siku ya tatu tangu kutokea kwa tukio hilo na
kuokolewa na askali polisi waliowahi kufika katika eneo la tukio,
wananchi hao walivamia nyumba ya bosi wake kisha kuibomoa na kuchoma
moto ambapo kikosi cha zimamoto kilifika na kufaninikiwa kuuzima moto
huo kabla ya kuiteketeza nyumba hiyo kabisa.
Askali wa jeshi la polis baada ya kufanikiwa na kuwadhibiti wananchi
kiatika kutekeleza uharifu huo
Mwenyekiti wa mtaa mzee Bukuku akiwataka wakazi wa eneo hilo kuondoka
na kuacha kuibomoa nyumba hiyo,
Zunda gabliel kaimu mkuu wa kituo cha polisi kati akiongea na wananchi
kufanya ulinzi wa nyumba iliyokua ikibomolewa
Henry kakobe askali wa kata ya Nonde akiwatuliza wananchi katika mkutano
ulioitishwa na mwenyekiti wa mtaa huo.
Wananchi waliofika kwenye mkutano wakitaka mtu aliehusika na mauwaji ya
mwanafunzi atajwe.
Askali kanzu wakiimalisha ulizi katika mkutano wa wananchi wa Nonde
Mbeya
Rebeka mwalyego afisa mtendaji wa mtaa wa mbwile (b) akiongea na
waandishi wa habari katika eneo la tukio
Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni