.

.

09 Aprili 2015

ACT-TANZANIA KUCHUKUA MAJIMBO YOTE KIGOMA KATIKA UBUNGE




Baada ya mijadala mingi kutoka kwa Zitto Kabwe na chama chake ACT-TANZANIA kuhusu kauli yake ya kwamba wabunge zaidi ya 50 walio katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania wataungana na chama chake  kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, ameonesha nia ya ACT-TANZANIA kutawala majimbo yote ya mkoani Kigoma.
“Nahitaji majimbo yote ya Kigoma kuchukuliwa na ACT bila kukosa hata moja na hili hata Serukamba (Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM) analijua. Mwanasiasa anayetaka kuwa mbunge Kigoma lazima aje ACT,” 

alisema Zitto ambaye pia alirejea kauli yake kuwa atagombea ubunge katika jimbo jingine lakini siyo Kigoma Kaskazini.


Kauli hiyo ya Zitto inawagusa wabunge wa sasa wa majimbo ya Kigoma ambao ni; Felix Mkosamali (Muhambwe), Moses Machali (Kasulu Mjini), Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) na David Kafulila (Kigoma Kusini), wote wa NCCR-Mageuzi na Peter Serukamba (Kigoma Mjini, Christopher Chiza (Buyungu) na Albert Obama (Manyovu) wa CCM.

Alipoulizwa iwapo wabunge hao wa majimbo ya mkoa huo ni miongoni mwa watu watakaohamia chama hicho alisema, 
“Sasa huo ni mtizamo wenu. Ukiwa mwanasiasa lazima uwe na msingi, nataka msingi uwe Kigoma.Tutakutana tena kwenye chumba hiki (cha mikutano) baadaye mwezi Novemba ili mnisute kwa kauli yangu na hapo itakuwa baada ya matokeo kutoka. Nahitaji kushinda kila kitu."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni