.
20 Aprili 2015
SERIKALI YA TANZANIA ITAWAREJESHA NYUMBANI RAIA 21
SERIKALI itawarejesha nyumbani raia 21 waishio kwenye kambi za hifadhi chini afrika ya kusini katika hatua yake ya kukabiliana na wasiwasi wa kushambuliwa kutokana na vurugu za chuki dhidi ya wageni zinazoendelea nchini humo.
Hata hivyo raia wengine 2 hawatohusishwa kwenye zoezi hilo la kurejea nyumbani kwa kuwa wameligomea.
Waziri wa mashauri ya kigeni Bernard membe amesema leo jijini Dar es salaam kuwa mpango huo wa kuwarudisha raia hao walioridhia umekamilika na utatekelezwa karibuni.
Vilevile membe amekanusha vikali kwamba hakuna raia yeyote wa Tanzania aliyefariki kutokana na visa vya kushambuliwa raia wa kigeni nchini afrika kusini ambavyo vimegharimu maisha ya watu 6 hadi sasa.
Mashambulizi dhidi ya wageni kwenye taifa hilo lililowahi kukumbwa na ubaguzi wa rangi yamezilazimisha nchi kadhaa barani afrika kuratibu zoezi la kuwatambua na kuwarejesha nyumbani mamia ya raia wao waishio afrika ya kusini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni