.

.

15 Mei 2015

MADAKTARI BINGWA WAPONGEZWA NA RAIS JK

JK awapongeza Madktari Bingwa wa Moyo kwa upasuaji


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na madaktari wa Shirika lisilo la kiserikali la Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza wanaoendesha zoezi la upasuaji na tiba ya moyo kwa zaidi ya watoto 70 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza akiwa katika picha ya pamoja na madaktari wa Shirika lisilo la kiserikali la Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza wanaoendesha zoezi la upasuaji na tiba ya moyo kwa zaidi ya watoto 70 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro
Mei 14, 2015 Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametembelea kitengo cha upasuaji wa moyo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwaona watoto ambao wamepata matibabu ya moyo kwa njia ya upasuaji na kuziba tundu la moyo bila kupasua, zoezi ambalo limeendeshwa na timu ya madaktari kutoka Taasisi ya Al Muntanda ya London, Uingereza, kwa kushirikiana na madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU imetayarisha video ya ripoti hii kuhusiana na ziara hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni